Habari za Punde

BONDIA ATOKA ULINGONI KUMGOMBELEZEA KAKA YAKE,PAMBANO LAVUNJIKA,MSUVA AGONGELEA MSUMARI

Mwanasoka wa Kimataifa Simon Msuva (kulia) akipozi kwa picha na Bondia Mfaume Mfaume kabla ya kuanza kwa pambano  la ubingwa wa Afrika Mashariki kati ya Mfaume Mfaume na Deo Samwel,lililofanyika katika Uwanja wa Kinesi usiku wa kuamkia jana. Msuva alimsindikiza Mfaume katika pambano hilo. 
Bondia Mfaume Mfaume (kushoto) akipambana na Deo Samwel wakati wa pambano lao la Round 10 laUbingwa wa Afrika Mashariki. Katika pambano hilo Mfaume alitangazwa mshindi baada ya kumpiga kichwa Deo na kuzuka vurugu uliongoni zilizomfanya Deo kutoka ulingoni na kwenda nje kugombelezea ugomvi wa kaka yake dhidi ya askari polisi na kugoma kurudi uliongoni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza wakati wa mapambano hayo
Bondia Mtanzania Feriche Mashauri (kulia) akipambana na Joyce Owino kutoka Kenya, wakati wa pambano lao la utangulizi la round 8 lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi usiku wa kuamkia jana kusindikiza pambano la round 10 la ubingwa wa Afrika Mashariki kati ya Mfaume Mfaume na Deo Samwel. Katika pambano hilo Feriche alishinda kwa pointi.
Feriche akitangazwa mshindi

Feriche akisubiri kuanza kwa pambano

Bondia Mkenya Joyce Owino akiimba wimbo wa Taifa lake kabla ya kuanza kwa pambano lake na Feriche huku akiwa amevaa bukta yenye bendera ya Tanzania kuonyesha anaipeza zaidi Tanzania kuliko nchi yake
Cosmas Cheka (kulia) akipambana na Habib Pengo, wakati wa pambano lao la utangulizi la round 8 lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi usiku wa kuamkia jana kusindikiza pambano la round 10 la ubingwa wa Afrika Mashariki kati ya Mfaume Mfaume na Deo Samwel. Katika pambano hilo Cosmas,  alishinda kwa pointi. 
Pambano la utangulizi
Baadhi ya viongozi wakiwa meza Kuu na Bondia Dullah Mbabe (kushoto)
Mwanasoka Simon Msuva akiwa ameketi na baadhi ya mashabiki wakifuatilia pambano la ngumi kati ya Mfaume Mfaume na Deo Samwel
Francis Miyeyusho (kulia) akipambana na Loren Japhet, wakati wa  pambano lao la utangulizi la round 8 lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi usiku wa kuamkia jana kusindikiza pambano la round 10 la ubingwa wa Afrika Mashariki kati ya Mfaume Mfaume na Deo Samwel. Katika pambano hilo mabondia hao walitoka sare. 
Japhet Kaseba (kushoto) akipambana na Mada Maugo. Maugo alishinda baada ya Kaseba kuumia mkono na kushindwa kumaliza pambano
Mashabiki wa ngumi wakiwa katika foleni kuingia uwanjani Kinesi kushuhudia mapambano ya ngumi.
Mara askari Polisi wakapanda ulingoni kutuliza vurugu kati ya mashabiki wa Mfaume na Deo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.