Habari za Punde

DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AAN KIKWAJUNI ZANZIBAR

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakati wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi, Salha Mohamed Khamis, baada ya kuibuka mshindi wa juzuu tano wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Saleh Nassoro Jazeera na Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia).
Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Salha Juma Sadalla akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.
Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kuwasili kiwanja cha Mapinduzi ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo visiwani Zanzibar.Wapili kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstari wapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya Kusoma Kurani baada ya kuwakabidhi zawadi.Mashindano hayo yamefanyika katika Kiwanja cha Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, akiwaaga wananchi (hawapo pichani), waliohudhuria hafla ya Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera. Picha na Mpiga Picha Wetu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.