Habari za Punde

KIKUNDI CHA BEAUTY WITH BRAIN,SERENA HOTEL WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KURASINI

 Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa wanawake cha Beauty with Brain cha jijini Dar es Salaam,Teddy Mapunda (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitabu mmoja kati ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Serikali kilichopo Kurasini,jijini Dar es Salaam,wakati kinamama hao kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena, walipotembelea kituo hicho leo asubuhi na kukabidhi Vyakula, Ndoo za rangi, Gipsum Board, Masweta ya watoto wote 71, nguo na viatu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Picha Zote na Nasma Mafoto 
 Mazungumzo kabla ya kukabidhi msaada huo
 Kina mama hao wakikabidhi sehemu ya msaada huo
Baadhi ya wafanyakazi wa Serena Hotel,wakiwa katika picha ya pamoja 
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Hoteli ya Serena, Sophia (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa tina za kuchanganyia rangi, msimamizi wa Kituo ya Yatima cha Kurasni, wakati kikundi hicho kilipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali leo asubihi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Beauty with Brain, Teddy Mapunda aliyeratibu safari hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.