Habari za Punde

KIPA WA KAGERA SUGAR JUMA KASEJA ASAINI KUITUMIKIA KMC MSIMU UJAO


ALIYEKUWA kipa wa Kagera Sugar, Juma Kaseja, amesaini mkataba wa mpya wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) iliyopanda ligi Kuu msimu ujao.
KMC ambayo imepanda daraja mwaka huu, ipo kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza Agosti mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, alisema kuwa wameamua kumsajili kipa huyo mzoefu ili aweze kuongeza nguvu na kuwapa morali vijana wa timu hiyo msimu ujao.
Aidha alisema kuwa kutokana na uwezo aliokuwa nao Kaseja wameona
anaweza kuisadia timu hiyo kufika mbali na hata kuchukua taji la ligi kuu.
"Kaseja ni mchezaji mzuri lakini pia ni pendekezo la kocha wetu Etienne Ndayiragije, kwani ameona uwezo wake pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu kwenye ligi kuu," alisema
Kwa upande wake kipa huyo, Kaseja alisema kuwa amefurahi kujiunga na timu hiyo na anawaahidi mashabiki na wapenzi wa mpira watarajie vitu vizuri kutoka kwake.
"Kwa sasa mimi ni mchezaji mpya wa KMC, naahidi nitaitumikia vyema timu yangu na kuipatia mafanikio mwanzo hadi mwisho wa msimu," alisema Kaseja
Mbali na Kaseja Kocha  Ndayiragije,pia amemchukua Nahodha wa timu yake ya zamani Mbao Fc, Yusuph Ndikumana na mchezaji wa Lipuli ya Iringa, Mussa Nampaka.
Sambamba na hao imeanza kazi ya kutaka kumnasa mchezaji mmoja ambaye amefahamika kwa jina la utani la Berbatov.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.