Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TANO KWA MTOTO LATIFA KADOGOSA ALIYEPOOZA MWILI JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-) fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya kiafya jijini Dar es Salaam. 
Katibu wa Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo  Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa Mwenge jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni Rehema Moyo akimkabidhi Kadi ya Benki Rehema Kadogosa mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha  nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.