Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AMJULIA HALI MSANII MAJUTO BAADA YA KUREJEA INDIA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe, wakimjulia hali msanii wa vichekesho, Mzee Majuto alipolazwa kabla ya kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi, ambapo amerejea nchini jana na kulazwa Hospitali ya Muhimbili. Picha na Maktaba
*******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAZIRI wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, jana mchana alikwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Msanii maarufu nchini,Amri Athuman maarufu King Majuto.
Majuto amelazwa katika hospitali hiyo baada ya kurejea nchini juzi akitokea nchini India.
Mzee Majuto anaendelea na matibabu baada ya kutoka India ambapo alikwenda kutibiwa.
Waziri Mwakyembe alikwenda kumjulia hali msanii ambapo King Majuto ameishukuru serikali kwa kumsadia.
King Majuto alikwenda India mwezi Mei, mwaka huu kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua karibu miezi mitatu .
Msanii huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, katika jiji la New Delhi.
Katika safari hiyo, Mzee Majuto aliambatana na mkewe Aisha Yusuf na mtoto wake wa kiume, Hamza

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.