Habari za Punde

JWTZ WATANGAZA AJIRA ZA MADAKTARI WA BINADAMU NA FANI ZA TIBA


Mkurugenzi wa habari na Uhusiano, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), Kanali Ramadhani Dogoli, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za jeshi hilo zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo mchana wakati akitangaza nafasi za ajira kwa Madaktari wa Binadamu, fani za Tiba. Kushoto ni Meja Lilian Ungani, kutoka Tawi la Utumishi. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
****************************
JESHI la Ulinzi  la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Tanzania katika kada ya Udaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika Makao makuu ya JWTZ , Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Kanali Ramadhan Dogoli, alisema nafasi hizo zimetolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali,vituo vya afya na Zahanati za JWTZ.
“ Jeshi limeamua kutangaza nafasi hizo kwa watanzania wote kuanzia miaka 18-28 ili kuongeza idadi ya wahudumu katika hosipitali,vituo vya afya na Zahanati zetu kulingana na mahitaji ya sasa na ya siku zijazo.Alisema”
Kanali Dogoli alizianisha sifa za waombaji hao, ambapo vijana wanaohitajika kujiunga na JWTZ ni wale walihitimu wa taaluma za Shahada za Udaktari katika madawa,meno,famasia na shahada ya mfumo wa utawala wa afya.
Shahada nyingine zitakazo hitajika ili kujiunga na JWTZ ni pamoja na shahada za udaktari katika maabara,muuguzi wa afya, na viungo na nyingine zinazohusu masuala ya afya.
Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo,raia wa Tanzania wakuzaliwa,umri kati ya miaka 18-28,awe na afya njema ya mwili na akili timamu,awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri,awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani nakufungwa jela.
Kadhalika muombaji anapaswa kuwa na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule, na vyeti vya vyuo alivyosoma na kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na kutunikiwa vyeti na awe amesajiliwa na bodi.
Taarifa hiyo pia imesema kwa wale ambao waliwahi kuhudumu katika Jeshi la Polisi,Magereza,Chuo cha mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo hawataruhusiwa kujiunga na JWTZ.
Wenye sifa tajwa na ambao wapo tayari kujinga na Jeshi hilo waripoti katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo,Mgulani Dar es Salaam tarehe 28,Agosti 2018 kuanzia saa1.00 asubuhi kwa ajili ya  usaili.
Hata hivyo JWTZ inawataka waombaji kujitegemea wenyewe kwa gharama za malazi,chakula na usafiri aidha watakaoandikishwa jeshini nakuchaguliwa watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao.
Mara tu watakapo jiunga na jeshi hilo watawajibika katika utekelezaji wa majukumu watakayopatiwa ambayo yatawapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.