Habari za Punde

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (Kkushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo kukagua namna inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Aunyisa Meena (kushoto), kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha miundombinu ya miradi ya hali ya hewa kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akifafanua jambo wakati kamati hiyo ikiwa katika ziara ya kujifunza namna  Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (kulia), akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya kujifunza namna mamlaka hiyo ivyofanya kazi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Seleman Kakoso na wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), katika chumba cha kutangazia taarifa za hali hewa, wakati kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bi. Hellen Msemo kutoka Mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.