Habari za Punde

MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
********************************************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali. 
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikiwasili katika ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani.
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikiwasili katika ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na furaha pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson wapili kutoka (kulia) pamoja na viongozi wengine wa Kidini na Serikali wakati ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ilipo tua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Muonekano wa Ndege Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitia sahihi pamoja na Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho kwa ajili ya makubaliano ambayo Serikali imeikodisha Ndege yake mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner kwa Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya kufanyia biashara ya usafiri wa anga.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner akijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
*Asema anaamini Watanzania wengi wanatambua umuhimu wa ndege hiyo 
*Asisitiza ujio wa ndege hizo zimenunuliwa kutokakana na kuziba mianya ya rushwa.
***********************************************
RAIS Dk. John Magufuli amesema ujio wa ndege mpya unafurahiwa na kila Mtanzania na kwamba yule ambaye haifurahii ajue atapa taabu sana huku akiwashukuru Watanzania wote kwa kufanikisha ujio wa ndege hizo. 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati anazungumza kabla ya ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ambapo amefafanua kuwa ujio wa ndege hizo unatokana na kutekeleza ahadi ya kufufua shirika la ndege nchini. Amesema katika juhudi hizo Serikali imeamua kununua ndege saba kwa fedha za Serikali na kwamba tayari ndege tatu zilishawasili nchini na leo ni ndege ya nne kuwasili nchini. 
“Mafanikio haya ni makubwa sana na niseme hajajileta yenyewe bali ni ya Watanzania wote.Nitumie nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote na kubwa zaidi anawashukuru kwa kulipa kodi kwani ndio imesababisha kununuliwa kwa ndege hizo saba. “Hivyo niwashukuru wote ambao wameshiriki katika ujio wa ndege hizi.Ukweli Watanzania tukiamua tunaweza na niishukuru Kamati ya Miundombinu kwa kukubali kununuliwa kwa ndege hizi na kuunga mkono juhudi zinazoendelea,”amesema Rais Magufuli. 
Ameongeza Serikali ya CCM iliamua kufufua shirika la ndege kuna sababu tatu , mowapo ni kurudhisha heshima ya Taifa kwani ilikuwa ni aibu kuwa nchi ambayo ina kila kitu halafu hakuna hata ndege ilikuwa ni aibu. “Tuliona tuanze kuitoa aibu hii ambayo tulikuwa tunaipata Watanzania.Kuna nchi ndogo lakini zina ndege lakini sisi hatukuwa nazo.Hivyo tuliona lazima tuiondoe aibu huu kwa kuwa na ndege. 
“Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege kwani mchango wake ni mkubwa na unahihitajika sana.Zipo sababu za watu kutopanda ndege ikiwamo ya kutokuwepo na miundombinu. “Sababu nyingine ya waanchi wengi kutopanda ndege ilikuwa ni gharama.Kwa watu wa Kagera wanafahamu kwenda Bukoba na kurudi ilikuwa ni Sh.milioni moja lakini sasa kupitia ndege za ATCL ni Sh.400,000,”amefafanua Rais. 
Pia amesema sababu ya kufufua ATCL ni kukuza utalii kwani Tanzania inashika nafasi ya pili duniani huku akifafanua pamoja na kuwa na vivutio vya utalii idadi ya watalii ni ndogo. Amesema hiyo inatokana na kukosekana kwa ndege kwani kote ambako wanapokea idadi kubwa ya watalii inatokana na uwepo na ndege za uhakika katika nchi zao. Mnapokuwa na ndege watalii wengi wanakwenda kuangalia utalii wanatumia ndege , hivyo hata uamuzi wa ndege hii ni kutaka kubeba watalii wengi. 
“Na ninaamini ndege hii itakapoanza kufanya kazi na ile nyingine itakapokuja itaongeza watalii,”amesema Rais Magufuli. Amesema amesikiliza maoni ya wananchi mbalimbali kutokana na ujio wa ndege hiyo ambapo wengi wameizungumzia vema na hivyo anwashukuru kwa ushirikiano wao. Pamoja na kuimarisha shirika la ndege ,Rais Magufuli amesema pia Serikali ya CCM inaendelea kuboresha usafiri wa majini , ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwamo madaraja na kwamba daraja linalojengwa Tazara litaitwa Mfugale. ia Rais Magufuli amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nishati ya umeme, miundombinu ya afya na elimu na kufafanua anaamini ifikapo mwaka 2025 Watanzania watakuwa katika uchumi wa kati. 
Rais Magufuli amesema maendeleo yanayopatikana sasa yanatokana na kuzima mianya ya rushwa na upotevu wa fedha kwani hivi sasa amebana upotevu wa fedha na matokeo yake fedha zinatumika katika kufanya maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.