Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU JULIUS NYERERE KINACHOJENGWA KIBAHA KWA MFIPA MKOANI PWANI.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, (wa nne kulia) Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomonisti cha watu wa China (CPC), Song Tao,pamoja na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vya Zanu Pf, ANC, Swapo, MPLA, CCM na Frelimo, kwa pamoja wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Kwa Mfipa Mkoa wa Pwani,leo mchana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO) 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu  wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa moja ya majengo ya chuo hicho katika mchoro kitakapokamilika kujengwa.
 Rais Magufuli akipongezana na Song Tao baada ya kuweka jiwe la Msingi
 Wakielekea kuwasalimia wananchi na kuburudika na bendi ya TOT
 Picha ya pomoja
  Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli ,Katibu Mkuu wa Chama cha Swapo cha Namibia, Sophia Shanangwa, wakipiga tumba katika jukwaa la Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika leo mchana Kwa Mfipa Mkoani Pwani.
 Wanamuziki wa bendi ya TOT, Abdul Misambano (kulia) na Kabatano, wakishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.
 Wanamuziki wa TOT waiimba jukwaani wakati wa hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Uongozi cha  Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.