Habari za Punde

TOT BAND YAKAMILISHA TATU MPYA, YAJIPANGA KUKIMBIZA KIVINGINE

 Baadhi yawanamuziki wa Bendi ya TOT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza shoo yao ya ufunguzi katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar esSalaam.
Bendi hiyo hivi sasa inaandaa nyimbo nyingine Nne zitakazokamilisha albam yenye jumla ya nyimbo sita ambapo tayari wamekwisharekodi nyimbo tatu mpaka sasa. 
Akizungumza na mtandao huu kiongozi wa bendi hiyo, Juma Jerry  'Jay Jay', alisema kuwa hivi sasa bado wanaandaa vibao vingine vinee ya muziki wa dansi vitakavyokuwemo katika albam hiyo.
Aidha alisema kuwa kutoka na ukimya wa muda mrefu bendi hiyo imejipanga kufanya mambo makubwa na kuwashangaza mashabiki wa muziki wa dansi na kurudisha heshima ya muziki huo.
Nyimbo hizo ni pamoja na Sabab Saba 42, Tendo Langu na Watanielewa tu iliyo katika miondoko ya Taarab taarab, ambazo zote zimerekodiwa katika Studio ya Hiland iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki mkongwe wa bendi hiyo aliyewahi kutamba na kibao cha taarab cha 'Asu' miaka ya nyuma.
Picha ya pamoja kwa pozi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.