Habari za Punde

TOT PLUS WAJIFUA KUJIANDAA NA CCM BONANZA FAMILLY, WAANDAA WIMBO MPYA WA MKUTANO WA CCM NA CPC

 Mwanamuziki wa bendi ya TOT Plus, Frank Almas 'Kabatano' akiimba na kuwaongoza wenzake wakati wa mazoezi ya bendi hiyo leo Mwananyamala kujiandaa na Bonanza la CCM Familly Bonanza linalotarajia kufanyika Juni 21 mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Ripota wa Mafoto Blog, Dar
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya Tanzania One Theatre  ToT Plus, imeandaa onyesho maalumu la CCM Familly Bonanza litakalofanyika Juni 21 mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Gazeti hili, Mkuu wa mipango na Uendeshaji wa bendi hiyo, Juma Jerry 'Jay Jay' alisema kuwa hivi sasa wapo katika mazoezi makali kujiandaa na onyesho hilo ambalo halitakuwa na kiingilio, ambapo pia litashirikisha bendi kongwe na maarufu za muziki wa dansi nchini.
Aidha alisema kuwa bonanza hilo ni maalumu kwa Viongozi na wanachama wa CCM, wananchi na hata wasio na vyama kwa ajili ya kukutana kubadilishana mawazo na kufurahi kwa pamoja huku wakipata burudani kutoka bendi mbalimbali zilizokwishathibitisha kushiriki bonanza hilo.
Alizitaja baadhi ya bendi zilizoalikwa katika Bonanza hilo kuwa ni pamoja na Twanga Pepeta, Fm Academia, Malaika Band, Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma, pamoja na wasanii mbalimbali wa Muziki wa Bongo Flava na Bongo Movie.
''Onyesho hili pia ndiyo litakuwa njia ya majadiliano kuurudisha muziki wa dansi katika nafasi yake kama ilivyokuwa zamani, nawahasa bendi washiriki kufanya mazoezi ya kutosha ili kuonyesha utofauti na kuwashawishi mashabiki kuamua kuishabikia bendi gani japo ni onyesho la ushindani lisilo na majaji'', alisema Jay Jay
Mbali na onyesho hilo pia bendi hiyo inaandaa wimbo maalumu kwa ajili ya mkutano mkuu wa Vyama tawala na rafiki vya AFrika unaoandaliwa kwa pamoja kati ya CCM na Chama cha Kikomonisti cha  China (CPC) na Uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo Kikuu cha Vyama vya Siasa litakalowekwa Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibaha hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.