Habari za Punde

TRC KUANZA KUFANYA MABORESHO YA RELI YA KATI KUPATA MWENDO WA KILOMETA 70 KWA SAA

Mratibu wa mradi wa uboreshaji wa Reli ya kati Dar es Salaam-Isaka, Mhandisi: Mlemba Singo, akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Shirika Tanzania Railways Corporation (TEC) lililopo ndani ya Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini, wakati akizungumzia kuhusu marekebisho ya njia hiyo ya Treni yatakayoiwezesha kutembea umbali wa Kilometa 70 kwa saa badala ya 35 kwa saa ambazo ni mwendo wa sasa. 

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Reli Tanzania, Jamila Mbarouk, akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wakitoa taarifa kuhusu mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati Dar - Isaka.
******************************************
Na Ripota wa MafotoBlog, Dar
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema katika maboresho ya reli ya kati litang'oa vyuma Km 312  vyenye uzani wa paundi 80 na kuweka vipya.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa Sabasaba vya Mwalimu Nyerere,  jijini Dar es Salaam, Mratibu Uboreshaji wa Reli ya Kati kutoka TRC, Mhandisi Mlemba Singo alisema, mradi wa Uboreshaji Reli ya Kati umewezeshwa na mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Alisema kwa sasa Reli imechakaa inahitaji maboresho makubwa wakati ujenzi wa reli ya kisasa ukiendelea.
"TRC imejipanga kuhakikisha usafiri wa treni  inakuwa wa uhakika ambao utarahisisha maisha na kukuza uchumi wa nchi," alisema Singo.
Singo alisema lengo la Uboreshaji Reli ya Kati ni kutoa usafiri wa kuaminika Na kukuza upatikanaji wa huduma bora nchini.
Alisema maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mizigo kutoka chini ya tani 13.5 ya uzito wa eskeli hadi gani 18.5.
Singo alisema pia watafanya ukarabati wa madaraja na makaravati 442, kuboresha mfumo wa mawasiliano, vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam, Ilala Na bandari kavu ya Isaka.
Alisema kupitia mradi huo imetengeneza mpango endelevu wa  matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya usafiri kuwa ya uhakika na kuaminika.
Kwa upande Meneja Uhusiano wa TRC, Fatma Mbarouk alisema, kuimarika kwa usafiri wa Reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo Serikali kuelekeza bajeti iliyotengwa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii.
Hata hivyo Mbarouk alisema.kabla ya kuanza ukarabati wa njia za Reli Juni mwaka huu. TRC. Imefanya kampeni ya uhamasishaji katika Mikoa ya Morogoro Pwani na Dar es Salaam ambapo ilitembelea wilaya za Kilosa, Mvomero, Morogoro vijijini, Manispaa, Kibaha vijijini na Wilaya ya Ilala.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.