Habari za Punde

VIGOGO WATANO WA KNCU LTD,TCCCO WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI

Watuhumiwa hao wakishushwa Mahakamani mapema leo chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polis,kusomewa mashtaka yao
Na Dixon Busagaga, Kanda ya Kaskazini
VIONGOZI watano wa Chama cha Ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU LTD) na Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Tanganyika (TCCCO) leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa Mashtaka tofauti yakiwemo ya uhujumu Uchumi.
Waliofikishwa Mahakamani na kupandishwa Kizimbani ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Kikuu cha Ushirika ,Kilimanjaro (KNCU) Aloisi Kitau (70) Makamu Mwenyekiti mstaafu wa KNCU,Hatibu Mwanga(70) na Meneeja Mkuu wa KNCU ,Honest Temba (38).
Wengine waliofikishwa mahamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi ,Pamela Mazengo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kukoboa Kahawa (TCCC0) Maynard Swai (57) na aliyekuwa Meneja Mkuu wa TCCCo ,Andrew Kleruu wanaotajwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mtambo wa kukoboa Kahawa.
Wakili wa serikali Jaqueline Nyantori aliieleza mahakamani kuwa Washitakiwa ,Maynard Swai na Andrew Kleruu wanakabiliwa na makosa mawili huku akiyataja kuwa ni Matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia serikali hasara .
Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mandamizi ,Shadrack Martin,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdalah Chavula na Wakili wa serijali Jacqueline Nyantori huku Wakili Julius Semali akimtetea Mshtakiwa Honest Temba na Wakili Captain Sawayaeli Shoo akimtetea Mshtakiwa Hatibu Mwanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.