Habari za Punde

WAZIRI KAMWELWE APOKEA KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe (wa tano kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wakishangilia kukamilika kwa zoezi la kupokea kivuko kipya cha MV. MWANZA. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe (katikati) akikata utepe uliofungwa kwenye kivuko cha MV. MWANZA kuashiria kukamilika mapokezi ya kivuko hicho. Kivuko cha MV. Mwanza kimeanza kazi ya kubeba abiria na magari, mara baada ya mapokezi hayo kukamilika.
 Waziri wa ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Isack Kamwelwe (wa nne kutoka kushoto) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela (kulia kwake) na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Brigedia Generali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri kupokea kivuko kipya cha MV. MWANZA kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza.
Kivuko kipya cha MV. Mwanza (kulia) kikiwa kimepaki katika maegesho ya Kigongo, kulia kwake ni kivuko cha MV. Misungwi ambavyo vyote kwa pamoja vina uwezo wa kubeba uzito wa tani 250, sawa na abiria 100 na magari 36 kwa wakati mmoja. Eneo la Kigongo/ Busisi sasa lina jumla ya vivuko vinne; MV. MWANZA, MV. MISUNGWI, MV. SENGEREMA pamoja na MV. SABASABA
Picha na THERESIA MWAMI - TEMESA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.