Habari za Punde

MAKAMBO ALIVYOWAHENYESHA MABEKI WA MTIBWA, YANGA IKISHINDA 2-1 TAIFA

 Vipi bwana mdogo, mikono ya nini tucheze mpira......, ndivyo anaokena kusema wakati Beki wa Mtibwa Sugar Is-Haka Hassan, akimghasi mshambuliaji huyo katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji mpya wa Yanga Eritier Makambo, akifunga bao la kichwa katika dakika ya 23 kipindi cha kwanza ambalo lilikataliwa na mwamuzi wa mchezo huo wa kwanza wa timu hizo katika ligi kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga wameshinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Eritie Makambo na Kelvin Yondani kipindi cha kwanza. 
 Makambo akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Mtibwa Sugar
 Makambo akishangilia bao lake halali la kwanza katika ligi Kuu.
 Makambo akikosa bao la wazi katika kipindi cha pili
******************************************

TIMU ya Yanga SC leo imeanza vyema mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC leo yalipatikana kipindi cha kwanza, yakifungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Eritier Makambo na Nahodha Kelvin Yondani kwa mkwaju wa penalti, baada ya Mrisho Ngasa kuchezewa faulo na Baba Ubaya ndani ya eneo la hatari wakati akielekea kumchungulia golikipa, huku bao la Mtibwa likifungwa na Haruna Chanongo aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Mtibwa Sugar waliuanza mchezo vizuri na kuutawala kwa takriban robo saa, kabla ya Yanga SC kuzinduka na kuanza kucheza vyema.
Wana Jangwani hao hawakukata tamaa na juhudi zao zikawalipa dakika ya 32, Makambo tena akifunga kwa kichwa tena akimalizia krosi ya beki wa kushoto Gardiel Michael.
Beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ akamuangusha mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa kwenye boksi na Yondan akaenda kufunga kwa penalti dakika ya 40.
Kipindi cha pili Yanga SC walikianza vizuri tena na Makambo akapoteza nafasi mbili nzuri za kufunga akiwa amebaki na kipa Benedictor Tinocco, mara zote akikosa hesabu nzuri za kumchenga mlinda mlango huyo.
Na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Chanongo akauwahi mpira uliopanguliwa na kipa Benno Kakolanya kuifungia bao pekee Mtibwa Sugar leo.
Bao hilo likawazindua Yanga na kuanza tena kupeleka mashambulizi langoni mwa Mtibwa Sugar, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi. 
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Stand United imeichapa 1-0 African Lyon Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati, KMV imelazimisha sare ya 0-0 na JKT Tanzania Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mchezo kati ya Azam FC na Mbeya City unaendelea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam kukamilisha mechi za ufunguzi za Ligi Kuu zilizoanza jana. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’ dk89, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Deus Kaseke, Feisal Salum, Heritier Makambo, Papy Kabamba Tshishimbi na Mrisho Ngassa/Raphael Daudi dk65.
Mtibwa Sugar; Beneditor Tinoco, Ally Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Hassan Isihaka, Shaaban Nditi, Ismail Aidan, Henry Joseph/Riffat Khamisi dk53, Kelvin Sabato, Awadh Juma na Salum Kihimbwi/Haroun Chanongo dk67.

 Ibrahim Ajibu (kulia) akijaribu 
 Beki wa Yanga Juma Abdul (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Mtibwa Sugar Issa Rashid
 Kaseke akipiga shuti huku akizongwa na mabeki wa Mtibwa Sugar.
 Kaseke akimiliki mpira
 Deus Kaseke, akiruka kikwepa kwanza la beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari 
 Winga wa Yanga, Mrisho Ngasa (kulia) akijaribu kumiliki mpira ili kumpita beki wa Mtibwa Sugar Cassian Ponera, wakati wa mchezo huo.
 Mrisho Ngasa akiruka kuwania mpira na beki wa Mtibwa Sugar

Wachezaji wa Yanga wakifurahia bao lao la pili, lililofungwa na Nahodha Kelvin Yondan (kulia) akikumbatiana na Kaseke.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.