Habari za Punde

SERENGETO BOYS YAKUBALI KIPIGO CHA 3-1 DHIDI YA UGANDA

 Kiungo wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys, Alphonce Msanga (kushoto) akichuna kuwania mpira na beki wa Uganda, John Alou,wakati wa mchezo wa Nusu Fainali wa U 17 kufuzu Afcon 2019, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es es Salaam, jioni ya leo. Katika mchezo huo Uganda wameshinda kwa jumla ya mabao 3-1 na kutinga fainali hizo ambapo watakutana na Ethiopia ambao pia wameweza kupenya katika mchezo wao dhidi ya Rwanda kwa mikwaju ya penati. 
Kwa hatua hiyo sasa Serengeti Boys itacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Rwanda.
 Mshambiliaji wa Serengeti Boys, Kelvin John, akiwania mpira na beki wa Uganda, Kizito Gavin.
 Nahodha wa Serengeti Boys, Morice Abraham, akiwatoka mabeki wa Uganda, Najib Yiga (katikati) na John Alou, wakati wa mchezo huo.
Alphonce, akiwatka mabeki wa Uganda. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.