Habari za Punde

TRC KUHAMISHA KITUO CHA TRENI CHA STESHENI KWA MUDA WA MIEZI NANE

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania, (TRC), Prof. John Kondoro, (wa tatu kushoto) akizungumza na baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika hilo, wakati walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa njia ya Treni ya umeme 'Standard Gauge' eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam, leo ambapo ziara hiyo ilimalizikia Kilosa mjini Morogoro. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Muonekano wa sehemu ya nguzo za mradi wa Standard Gauge zilizojengwa eneo la Shauri Moyo.
Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa, akizungumza wakati wa ziara hiyo.
***************************************
Na Sufianimafoto Ripota
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limebadili kituo cha mwanzo na mwisho wa safari zake za Treni kuanzisha keshokutwa kwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Ubungo na ile ya Stesheni Gongolamboto ambazo kwa sasa zitaanzia na kuishia eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam, ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, leo Mkurugenzi Mtendaji Masanja Kadogosa amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya kuboresha eneo la Shauri Moyo na ambapo kesho  wanatarajia kukamilisha mahitaji yote muhimu katika kituo hicho cha Shaurimoyo na baada ya hapo hapo ndipo itakuwa Shesheni ya treni hizo sambamba na ile ya mkoani.
"Hivyo wananchi wanaotumia usafiri wa treni za Dar es Salaam badala ya kuanzia Stesheni na kuelekea Ubonga au Gongolamboto sasa watakuwa wanapanda au kushuka eneo la Shauri moyo,"alisema.
Aidha, Kadogosa alisema sababu za kuhamishia Stesheni hiyo ya Shauri moyo ni kupisha ujenzi wa Stesheni ya Reli ya Kisasa ambayo ujenzi wake unaendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 22.
Kesho tunakamilisha ujenzi wa eneo hili la Shauri Moyo na kesho kutwa treni zetu zitakuwa zikianzia safari zake hapa na kumalizia hapa.
Tunawaomba wananchi wafahamu kuwa Stesheni tunataka kuanza ujenzi wa kituo cha ya Reli ya Kisasa 'Standard Gauge' ambapo ujenzi huo unatarajia kuchukua kati ya miezi sita hadi nane.
Kadogosa amewahakikishia wananchi wanaotumia usafiri huo kwamba usalama upo wa kutosha na kutakuwa na utaratibu mzuri wa kutoa 
maelekezo yakiwamo ya mageti ya kuingia na kotokea.
Ameongeza kuwa wanatambua licha ya kuhamishia Stesheni Shaurimoyo bado kuna ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea, hivyo wamechukua tahadhari zote.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Profesa John Kondoro baada ya kuelezwa taarifa hizo za kuhamishwa kwa Stesheni kutoka ilipo na kuhamishiwa Shaurimoyo alitaka kufahamu usalama wa abiria , ambapo amethibitishiwa na Kadogosa kwamba usalama utakuwepo.
Profesa Kondoro alifika eneo la Shaurimoyo akiwa ameongozana na wajumbe mbalimbali wa bodi yake ambao walifika hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa unaondelea.

Meneja msaidizi wa mradi huo, Chedi Masambaji, akifafanua jambo kuhusu ujenzi huo.
 Wakitembelea mradi huo.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Chananja Muhandikila, kuhusu ujenzi wa Mradi wa njia ya Treni ya umeme 'Standard Gauge' eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mradi Mhandisi Maizo Bugedzi, kuhusu ujenzi wa Mradi wa njia ya Treni ya umeme 'Standard Gauge' eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakiangalia moja ya eneo linalochimbwa ili kujengwa njia ya Treni ya umeme 'Standard Gauge' eneo la Pugu.
 Maandalizi 
 Mafundi wakiendelea na maandalizi ya Reli ya Kati eneo la Shaurimoyo kwa ajili ya kituo cha Stesheni kuhamia eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.