Habari za Punde

TANI 7,250 ZA RELI YA KISASA ZAWASILI DAR, KUPELEKWA SOGA KUANZA KUTANDIKWA

 Kaimu Meneja Masoko TRC Never Diamon (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani (katikati) wakati walipokuwa wakikagua Tani 7,250 za Reli zilizowasili na Meli ya Finesse kutoka nchini Japan kwa ajili ya kutandika katika Kilometa 60 za njia ya Treni ya kisasa ya Dar es Salaam mpaka Morogoro, ambayo ni sawa na asilimia 20 ya ujenzi huo. Ukaguzi huo umefanyika katika Bandari ya Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Ofisa habari wa TRC Jamilla Mbarouk. 
 Meneja mradi wa Reli ya kisasa 'Standard Gauge', Eng. Maizo Mgedzi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani, wakitoka kukagua jumla ya Tani 7,250 za Reli zilizowasili na Meli ya Finesse kutoka nchini Japan kwa ajili ya kutandika katika Kilometa 60 za njia ya Treni ya kisasa ya Dar es Salaam mpaka Morogoro, ambayo ni sawa na asilimia 20 ya ujenzi huo. Ukaguzi huo umefanyika katika Bandari ya Dar es Salaam
 Sahani akifafanua jambo kuhusu upakuaji wa Reli
 Sehemu ya Reli hizo zikiwa katika Meli ya Finesse
Maelekezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.