Habari za Punde

BONDIA HASSAN MWAKINYO ATANGAZWA BALOZI WA SPORTPESA TANZANIA

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akishuhudia Mkurugenzi wa Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Bondia Hassan Mwakinyo, wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika kwenye Ofisi za Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
**************************************************************
KAMPUNI ya ubashiri michezo ya SportPesa Tanzania imeingia mkataba wa udhamini na Bondia Hassan Mwakinyo mwenye uzani wa Super Welter anayeongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika mchezo wa ngumi na kumtambulisha kama Balozi wa Kampuni hiyo kwa miaka mitatu.
 WaziriI wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akishuhudia Mkurugenzi wa Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba (wa pili kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Bondia Hassan Mwakinyo, wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo liyofanyika kwenye Ofisi za Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, leo Kushoto ni Mwenyekiti wa TPBRC, Joe Joseph.
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba (wa tatu kushoto) na bondia Hassan Mwakinyo (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi baada ya kusainiana mkataba wa udhamini wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika kweny Ofisi za Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPBRC, Joe Joseph. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.