Habari za Punde

KAMWELWE AFUNGUA MAFUNZO YA UDEREVA WA TRENI YA UMEME

 Waziri wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe, akifungua rasmi mafunzo ya udereva na usimamizi wa Treni ya Umeme ya Kisasa inayojengwa nchini chini ya mradi wa Reli ya Kisasa (SGR). Mafunzo hayo ya awamu ya pili yaliyoshirikisha washiriki 33 wake kwa waume yalifunguliwa leo jijini Dar es Salaam. 

 Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akizungumza jambo katika mafunzo hayo.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo, ambapo jumla ya washiriki ni 33 kati yao wanawake ni watano, wanne ni upande wa madereva na mmoja ni Steshen Master.
 Waziri wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya udereva na usimamizi wa Treni ya Umeme ya Kisasa inayojengwa nchini chini ya mradi wa Reli ya Kisasa (SGR). Mafunzo hayo ya awamu ya pili yaliyoshirikisha washiriki 33 wake kwa waume yalifunguliwa leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC, Kondoro na Mkurugenzi wa TRC Masanja kadogosa, wakimsikiliza Meneja wa Kampuni ya Yapi Merkez Kanda ya Afrika Mashariki, Mhandisi Abdullah Kilic, wakati akifafanua jambo kuhusu darasa la mafunzo ya udereva na usimamizi wa Treni ya Umeme ya Kisasa inayojengwa nchini chini ya mradi wa Reli ya Kisasa (SGR). Mafunzo hayo ya awamu ya pili yaliyoshirikisha washiriki 33 wake kwa waume yalifunguliwa leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.