Habari za Punde

GENERATION QEENS WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA KITUO CHA AFYA CHALINZE

 Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Qeens Bety Msimbe kulia akimkabidhi msaada wa vifaa mbali mbali   mmoja wa wakinamama  Zulfa Athumani katika halfa fupi kwa niaba  ya wengine  baada ya kujifungua  katika kituo cha afya chalinze kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
 Baadhi ya viongozi na wanachama wa kikundi cha Pwani Generation Qeens wakiwa ndani ya kituo cha afya chalinze ambapo walifanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa na kutoa msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia wakinamama wajawazito pamoja na watoto.
Kikundi cha Pwani Generation Qeens kikiwa katika picha ya pamoja nje ya wodi ya wazazi katika kituo cha afya chalinze mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa vifaa mbali mbali kwa wanawake  wajawazito na watoto.
********************************
 VICTOR  MASANGU, CHALINZE
 KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito pamoja na watoto wachanga kikundi cha  Pwani Generation Qeens kimetoa msaada wa vifaa mbali tiba  mbali katika kituo cha afya Chalinze kilichopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  kwa lengo la  kusaidia  kutatua changamoto ambayo ilikuwa inawakabili wanawake  wakati wa kujifungua.
Akikabidhi msaada wa vifaa tiba mbali mbali katika kituo hicho cha afya  Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Qeens Bety Msimbe alisema kwamba wameamua kutoa msaada katika wodi ya wazazi kutokana na kubaini kuwepo kwa  uhaba wa vifaa tiba hasa kwa wanawake  wajawazito ambao wanakwenda kupatiwa matibabu.
Aidha Msimbe alisema  kwamba  kumekuwepo na baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakipata shida sana  pindi wanapokwenda katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali kwa ajili ya kujifungua hivyo wakaona kuna umuhimu wa kutoa msaada huo  ambao utawasaidia  wakinamma wajawazito, waliojifungua  pamoja na watoto wachanga.
Nao baadhi ya wanawake ambao wamenufaika na msaada huo akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja  walisema  kwamba ni kweli wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa kwa ajili ya kujifungulia  na wakati mwingine inawalazimu kwenda dukani kununua ukizingatia baadhi yao  uwezo wao wa kifedha ni  mdogo hivyo  wanashindwa kumudu gharama za matibabu.
“Kwa kweli kwa upande wetu kama wanawake tumefarijika sana na msaada huu kutoka katika kikundi cha Pwani Generation Qeens maana changamoto yetu ilikuwa ni vifaa tiba pamoja na mahitaji mbali mbali hasa wakati wa kujifungua maana wakati mwingine tunajikuta tunakosa vifaa muhimu na wakati mwingine tunanunua,”walisema.
Kwa upande wake  Mganga mfawidhi wa kituo cha afya chalinze Salama Masukuzi
amebainisha  kwamba changamoto  zinazowakabili kwa sasa ni kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wagonjwa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa majengo ya wodi za wazazi  pamoja na  vitanda  na kupelekea wakati mwingine wagonjwa kuwalaza wawili  katika kitanda kimoja.
Aidha alisema kwamba  pamoja na kukabiliwa na changamoto hizo pia kuna upungufu wa madaktari pamoja na wauguzi hivyo kupelekea kufanya kazi katika mazingira magumu  kutokana na kupokea idadi kubwa ya wagonjwa hivyo ameiomba serikali kuwaboreshea zaidi huduma ya afya kwa ajili ya kuweza kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.