Habari za Punde

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO KUANZA KUTOA ASTASHAHADA NA SHAHADA ZA DAWA ZA BINADAMU NA MIFUGO


 Baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian wakiongozana na mgeni rasmi kuwasili katika sherehe ya maafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo. Picha na Mafoto Media
 Baadhi ya wahitimu wa  stashahada na Shahada ya Elimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCO) wakifurahia na kupiga makofi wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo mkoani Pwani. 
Baadhi ya wahitimu wa  stashahada na Shahada ya Elimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCO) wakifurahia na kupiga makofi wakati wa sherehe ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo mkoani Pwani. Picha na Mafoto Media
********************************************************

Na Scolastica Msewa, Bagamoyo
CHUO Kikuu kishiriki cha Marian  MARUCO kina mpango wa kuanza kutoa astashahada na shahada za kutengeneza dawa za binadamu na dawa za mifugo ili  kufikia ufanikishaji wa juhudi za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Muhasham Askofu Antony Banzi wa jimbo katoriki tanga mwakirishi wa chuo kishiriki cha St. Agustino amesema hayo katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo mkoani Pwani ambapo jumla ya wahitimu 326 walitunukiwa astashahada na shahada za masomo ya sayansi.
Alisema Tanzania imekuwa ikitilia mkazo mkubwa sana katika utoaji wa elimu na upanuzi wa wigo wa elimu ili kuwezesha watanzania wengi kupata elimu kuanzia ngazi msingi hadi elimu ya juu na ndio msingi wa mafanikio ya kuleta maendeleo katika taifa lolote duniani ikiwemo Tanzania.
Alisema katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa viwanda kama ilivyoainishwa katika dira ya maendeleo ya taifa 2025 MARUCO imeazimia kutekeleza mpango kazi wake wa miaka mitano (2015-2020) ili kuunga mkono juhudi za serikali za kupata wataalamu wenye sifa stahiki kwa kuanzisha program mpya katika ngazi ya shahada ya kwanza, uzamili na uzamivu katika Nyanja mbalimbali za sayansi na tekinolojia.
Muhasham Askofu Banzi alisema pia chuo kimepanga kufundisha kozi ya sayansi ya viumbe na mimea ya bahari hasa kwa kuwa chuo hicho kipo karibu na bahari Hindi hivyo watatumia malighafi hiyo katika kufundishia.
Program nyingine ni pamoja na kuanzisha masomo ya nyanja ya nishati mbadala, usalama wa mitambo na sayansi ya madawa, elimu ya elektroniki kwa ajili ya kubuni, kuunda na kukarabati vifaa vya elektroniki.
“Mpango mkakati mwingine ni pamoja na kutoa elimu ya hesabu na Bima, hesabu na uchumi kozi zitakazo mwezesha muhitimu kuchangia kikamilifu katika sekta ya biashara na viwanda nchini” alisema Muhasham Askofu Antony Banzi.
Alisema pia chuo hicho kina mpango wa kupanua na kujenga miundombinu mipya ili kukiwezesha chuo kudahili wanafunzi wengi zaidi, kuboresha utafiti katika maeneo mbalimbali ya sayansi na kuimarisha ushirikiano na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kushirikiana katika kubadilishana uzoefu na kufanya tafiti za pamoja.
Mkuu wa chuo kikuu kishiriki cha Marian Profesa Peter msolla aliwataka wahitimu hao kuwa mabarozi wema wa kukitangaza chuo kwa uwezo wao wa kitaaluma, kwa tabia, uadilifiu na uchapa kazi ili kuweza kukithi katika soko la ajira na kujiajiri ili kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Alisema matarajio ya chuo hicho ni kuendelea kupanua udahili wa wanafunzi na kuongeza idadi yao, kuboresha mafunzo, utafiti, ushauri na huduma za kitaaluma katika jamii.
Profesa Msolla alisema kati ya wahitimu 326, 325 ni wa shahada za kwanza na mmoja ni wa astashahada.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.