Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA SHEREHE ZA MADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR-PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kuwasalimia wananchi waliofurika katika Uwanja wa Gombani mjini Pemba wakati akiwasili uwanjani hapo leo kuhudhuria Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Muhidin Sufiani) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika Uwanja wa Gombani Pemba katika sherehe za Kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo.
 Askari wa JWTZ Makomandoo wakionesha umahili wao kwa kupambana bila silaha wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi wa Zanzibar. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Vijana wa kikundi cha Uhamasishaji wakipita na maandamano mbele ya Jukwaa kuu wakiwa na Picha za Viongozi wa Tanzania Bara na Visiwani wakati wa sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi, kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba. 
 Askari wa Jeshi la Kikoloni Tarabushi wakipita mbele ya Jukwaa kuu. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kama ishara ya kupokea maandamano.
 Katibu Mkuu wa CCM Bara, Dkt Bashiru (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria sherehe hizo kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba.
 Askari wa JWTZ kikosi cha Makomandoo wakipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe hizo.
 Katibu wa Vijana wa CCM mkoa wa Pwani (mwanadada katikati mbele) akiwaogoza vijana wenzake wa CCM kupita mbele ya jukwaa kuu wakati wa sherehe hizo.
 Askari wa JKU wakipita mbele ya jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohame Shein, wakati wa sherehe hizo.
 Askari wa Jwtz wakipita mbele ya jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohame Shein, wakati wa sherehe hizo.
 Askari wa KMKM wakipita mbele ya jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohame Shein, wakati wa sherehe hizo.
 Askari Polisi wanawake wakipita mbele ya jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohame Shein, wakati wa sherehe hizo.
 Maandamano
 Vijana wa kikundi cha Uhamasishaji cha CCM wakipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa ujumbe wao kwa mgeni rasmi.
 Sehemu ya Viongozi na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.
Taswira ya uwanjani
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia SUluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Bara, Dkt. Bashiru na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Philp Mangula, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Gombani Pemba kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Phillip Mangula, akiwasili kwenye Uwanja wa Gombani Pemba katika sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi 
 Sehemu ya Viongozi na wageni waalikwa.
 sehemu ya wananchi
 Makamu wa Rais akiwasili
 Waziri Mkuu akiwasili
 Wageni na Mabalozi wakiwasili
 Wananchi
Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya jukwaa kuu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.