Habari za Punde

MBUNGE KIGODA ACHANGIA MILIONI 24 UJENZI WA MADARASA MJI WA HANDENI

Mbunge wa Handeni Mjini, akipiga Sululu wakati wa zoezi la MSALAGAMBO wananchi kujitolea kuchimba msingi wa Vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Handeni.  Picha na Muhidin Sufiani.
MBUNGE wa Jimbo la Handeni Mkoa wa Tanga, Omary Abdallah Kigoda, ametoa jumla ya Sh. milioni 24 kwa ajili ya kuchangia Kazi za kujitolea katika maendeleo (MSALAGAMBO) unaoendelea katika jimbo lake kuinua sekta ya elimu na kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati jimboni kwake.
Wananchi wa jimbo hilo wamepata hamasa kubwa na kujotokeza kwa wingi katika kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa ili kuondoa upungufu wa madara katika shule za Sekondari.
Akizungumza na Uhuru wakati wa uchimbaji msingi wa Vyumba vya viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Handeni, Mbunge, Kigoda alisema kuwa kwa wananchi kuchangia chochote ili kufanikisha jambo hilo.
Aidha Kigoda alisema kuwa hadi sasa kuna upungufu wa madarasa 13 katika jimbo hilo katika shule za Sekondari ambapo tayari wameanza mpango wa kujitolea ili kupunguza changamoto hiyo kubwa inayowakabili katika jimbo lake, ambapo wameamua kuanza na ujenzi wa madarasa mawili kila shule.
Shilingi milioni 24 zilizotolewa na mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Kigoda katika mfuko wajimbo zitatumika kununua vifaa vya ujenzi vya viwandani ikiwa ni pamoja na mabati, misumari, mbao n.k.
Pia Kigoda aliishukuru Serikali ya Mji wa Handeni kuahidi kusimamia matumizi ya fedha hilo kuhakikisha zinatumika ipasavyo kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo, unaotarajia kukamilika mapema mwezi Februari.
Katika mchakato huo Mbenge na wananchi wake wana mpango wa kujenza madarasa manne katika shule hiyo ya Handeni Sekondari ambapo wameanza na madarasa mawili huku wananchi wakijitolea nguvukazi, Pesa ama vitu vyenye thamani na pesa ili kufanikisha jambo hilo.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, Mwalimu Boniface Maige, aliwashukuru na kuwapongeza viongoz, wananchi kujitokeza kwa wingi na Wabunge wa Wilaya ya hiyo Ombary Abdallah Kigoda, mbunge wa Handeni mjini, aliyechangia kiasi cha Sh Milioni 24 na Mboni Muhita Mbunge wa Handeni Vijijini, aliyechangia Sh. milioni 19 huku Msalagambo huo ukianzia Kata ya Mkata, Kabuku na Kivesa.
Katika Wilaya yetu ya Handeeni tuna upungufu wa madarasa 62 kwa wilaya nzima ya Handeni ambapo kwa Handeni Wilaya kuna upungufu wa madarasa 49 na Handeni mjini kuna upungufu wa vymba vya madarasa 13, mpaka sasa tayari wameshaandaa jumla ya vyumba 50 vilivyoanza kujengwa na wananchi ambapo kwa wikiendi iliyopita Msalagambo huo umefanyika katika Shule za Sekondari Handeni, Kwenjugo na Maili Kumi.
Aidha aliwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia kwa wingi ili kufanikisha mchakato huo wa kuondoa upungufu wa madarasa katika Wilaya ya Handeni ambao umeshika kasi na kuungwa mkono na viongozi na wanachi wa Wilaya hiyo.
''Tutakuwa tumepiga hatu zaidi katika Mkoa wa Tanga na hasa Wilaya yetu ya Handeni katika Sekta ya Elimu, iwapo tukiendelea kushirikiana kwa nguvu moja kama hivi na wadau wengine wakijitokeza kuchangia ili watoto wetu waweze kusoma bila matatizo wakiwa ndani ya vyumba vya madarasa''. alisema Maige

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.